Algeria imesitisha shughuli za
kandanda kwa kipindi kisichofahamika kufuatia kifo cha mchezaji kutoka
Cameroon, Albert Ebosse aliyekufa baada ya kurushiwa kitu na mashabiki.
Shirikisho la kandanda la Algeria limefikia uamuzi huo siku ya Jumapili.
Ebosse, 24, aligongwa na kitu kichwani wakati akitoka uwanjani baada ya
mechi kumalizika kati ya timu yake JS Kabylie iliyofungwa na USM Alger
siku ya Jumamosi, jijini Tizi Ouzou. Mamlaka za Algeria awali zilikuwa
zimeufungia uwanja wa Novemba Mosi 1954 lilipotokea tukio hilo. Amri
hiyo sasa inajumuisha viwanja vyote nchini humo. Shirikisho hilo pia
limesema litatoa dola 100,000 kwa familia ya Ebosse, kiasi ambacho
angelipwa katika muda wa mkataba wake. Zaidi ya hilo, wachezaji wa JS
Kablylie, kila mmoja atatoa mshahara wa mwezi mmoja.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!
Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com ! Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...
-
UTANGULIZI. Uyoga ni aina ya nyuzi kuvu (fungus) yenye kutofautiana na mimea mingine kwa kukosa chembe chembe zinazowezesha mimea ku...
-
Kutoka Jiji la Chicago Nchini Marekani Kijana wa Kiume Micah ambaye ni msanii wa R&B anayechipukia mwenye umri wa miaka 20 amechuk...
No comments:
Post a Comment