welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Wednesday, 27 August 2014

C.E.O WA WIMBO WA NITASUBIRI JUX - ASHINDWA KUSUBIRI NA KUKATA TAMAA MAPEMA

JUX NA V-MONEY

Jux na Jackie
aliemuimbia nitasubiri ambapo
uvumilivu umemshinda kabisa
MBONGO-Fleva anayefanya poa na ngoma yake ya Nitasubiri, Juma Mussa ‘Jux’ na staa mwenzake ambaye ana kofia nyingine ya utangazaji, Vanessa Mdee ‘V-Money’ wanadaiwa kuwa ni wapenzi, Risasi Jumatano limeinyaka.
Madai ya wawili hao kuhusishwa kimapenzi yameendelea kujidhihirisha siku hadi siku na zaidi ni hivi karibuni walipokutana kwenye ziara ya Serengeti Fiesta 2014 mkoani Kagera na Tanga, ambapo muda mwingi walionekana kugandana kama luba hadi wenzao kudai kuwa walikuwa hata wakilala chumba kimoja hotelini.
Katika kuwafuatilia, mwanahabari wetu alifanikiwa kupata baadhi ya picha za matukio yao yaliyoonesha michakato na harakati zao za kimalovee zinavyokuwa siku zote.


  Jux na Vanessa, wakiwa mkoani humo walionekana muda mwingi wakiwa pamoja kwenye gari walipokuwa wakienda kumuona Babu Njenje na wakati wakiwa wanaelekea Uwanja wa Mkwakwani kwenye shoo.
Hata baada ya Jux kushuka stejini, alionekana akiwa amekaa ‘very close’ na Vanessa huku wakiwa kwenye mazungumzo yaliyodaiwa ni ya kimahaba niue.


 Mwandishi wetu alifanya jitihada za kuzungumza na Jux juu ya uhusiano wao, lakini jamaa huyo alimchomolea kwa kusema kwamba hayuko tayari kuzungumzia ishu hiyo kwani Vanessa ni mshikaji wake tu na hakuna kibaya juu yao zaidi wanafanya kazi pamoja tu.
“Kiukweli sihitaji kuzungumza lolote juu yangu na Vanessa ila ni mwanamuziki mwenzangu hivyo tunafanya kazi pamoja,” alisema Jux.Vanessa kwa upande wake alipoulizwa juu ya ishu hiyo, alimtaka mwandishi wetu ‘kuipotezea’ habari hiyo kwani si muhimu kwa sasa.

 Mbali na Vanessa, Jux aliwahi kudaiwa kutoka na mwigizaji Jacqueline Wolper na modo Jacqueline Patrick huku Vanessa naye akiwa alisharipotiwa kutoka na Omary Nyembo ‘Ommy Dimpoz’.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...