Miaka
miwili baada ya kufunga pingu za maisha (ndoa) na mwanaume aitwaye
Kauli Juma, imefichuka kwamba ndoa ya prizenta wa Star TV, Sauda Mwilima
ina shida kwani haishi na mumewe, ikidaiwa kwamba kila mmoja anaishi
nchi tofauti na mwenzake.Kikizungumza
na Ijumaa Wikienda, chanzo makini ambacho ni mtu wa karibu wa Sauda,
kilisema kwamba baada ya wawili hao kufunga ndoa, Kauli aliondoka kwenda
nchini Afrika Kusini ‘Sauzi’ alikokuwa akifanya shughuli zake kabla ya
kufunga ndoa na hadi leo hajawahi kurudi Tanzania.
“Hata alipojifungua na mtoto kufariki dunia kwa bahati mbaya, mumewe hakuwepo na hadi leo hajarudi, ukweli inauma sana ila Sauda ni mvumilivu kwani ndoa yake ni shida,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kuzinyaka habari hizo, mwanahabari wetu alimtafuta Sauda ambapo alikuwa na haya ya kusema:“Ni kweli anaishi Sauzi. Tangu tukiwa wachumba tulielewana kwamba tukioana kila mtu ataendelea kuishi anapoishi hivyo mume wangu anafanya shughuli zake nchini Afrika Kusini na huwa anakuja mara mojamoja akiwa na nafasi au akiwa likizo.

“Mimi
siyo mtu wa kujionesha kwamba eti mume wangu yupo nchini hivyo akija
huwa ni kimyakimya anakaa tunaendelea na mambo ya familia yetu basi muda
ukiisha anaondoka na tulikubaliana tangu tukiwa wachumba hivyo ikitokea
mmoja wetu ameamua kumfuata mwenzake na kwenda kuishi naye hakuna
shida,” alisema Sauda.Sauda aliongeza kwamba ndoa yake iko vizuri na hawajaachana na endapo ingekuwa haipo asingevaa pete ya ndoa.
“Ndoa yangu haijavunjika, tuko vizuri na mume wangu japokuwa tuko mbali lakini kila mmoja anamwamini mwenzake,” alisema Sauda.
Wadau wanaifananisha ndoa hiyo na ya Aunt Ezekiel na kudai kuwa wawili hao hawachekani
“Ndoa yangu haijavunjika, tuko vizuri na mume wangu japokuwa tuko mbali lakini kila mmoja anamwamini mwenzake,” alisema Sauda.
Wadau wanaifananisha ndoa hiyo na ya Aunt Ezekiel na kudai kuwa wawili hao hawachekani
No comments:
Post a Comment