Mambo
yanazidi kupamba moto baada ya uongozi wa Yanga kusema ulipeleka jina
la mshambuliaji Emmanuel Okwi katika majina yake ya wachezaji.Yanga
imesema ilipeleka jina hilo, hivyo inashangazwa kusikia Simba
imemsajili na imeamua kuongeza adhabu ya kutaka afungiwe na ile faini
kutoka dola 200,000 iongezeke nyingine ya dola 500,000.
Kama
hiyo haitoshi, Mwenyekiti wa Yanga, Yusuf Manji amewaambia waandishi wa
habari leo jijini Dar kwamba walituma barua ya kutaka kuvunja mkataba
kwa TFF wakieleza nia yao.
“TFF haikuwa bado imejibu, Okwi akatuandikia sisi barua lakini sisi hatukiandika kwake. Ilipaswa naye apelike TFF.
“Simba
pia wamefanya kosa, wanajua Okwi bado ana mkataba na Yanga, lakini
wamekurupuka na kumsajili ambalo ni kosa kwa mujibu wa Fifa na Caf.
“Yanga
tunajua bado suala la wachezaji wa kigeni liko wazi, dirisha
halijafungwa. Ndiyo maana tulipeleka jina lake tukijua kama suala la
kupunguza mchezaji mmoja litafika, tutalifanyia kazi.
“Simba
na Okwi, wote wanapaswa kufungiwa kutokana na kukiuka vipengele hivi.
Sisi tuliamini ni watu wa busara ambao wanakuja kuendeleza soka, lakini
hizi ni vurugu ambazo hazijengi,” alisema Manji.
“Tunaamini suala letu TFF italishughulikia ndani ya siku saba, ikishindikana tukakwenda Caf, Fifa au Cas (mahakama ya soka).”
HAYA NDIYO INAYASISITIZA YANGA KWA OKWI:
1. Tokea
lakini laki 2 hadi laki 5, Simba pia inawahusu, wasingekubali,
wangefuata utaratibu, wamemfuata mchezaji kabla ya kuanza na timu.
2. Wataiomba TFF, ikiwezekana Okwi afungiwe kucheza moja kwa moja, pia Simba kwa kuwa wamemsajili akiwa bado na mkataba.
3. Hawajavunja mkataba, barua aliyoiandikia Yanga, ilitakiwa aindikie TFF kwa kuwa yenye haikumuandikia yeye.
4. Wametoa siku 7 kwa TFF kusikiliza na kutoa majibu ya kesi yao, la sivyo watalipeleka Caf, Fifa au Cas.
No comments:
Post a Comment