welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Sunday, 24 August 2014

SOMA ALICHOSEMA BOSI WA MANCHESTER UNITED:


KUSHINDA LIGI ITAKUWA MAAJABU-
 Boss wa Manchester United Louis van Gaal amesema itakuwa "maajabu" kama timu yake itashinda ligi kuu ya England msimu huu.
LOUIS VAN GAAL
United wanacheza na Sunderland Jumapili, -baada ya kupoteza mchezo wa kwanza wa ligi dhidi ya Swansea.
Van Gaal, 63, anajaribu kurekebisha kikosi "kisicho na uwiano", huku klabu hiyo ikigoma kabisa kuzungumzia uhamisho wa Angel Di Maria kutoka Real Madrid.
"Kushinda ligi msimu huu itakuwa maajabu. Lakini sisemi kuwa haiwezekani," amesema Van Gaal.
Kocha huyo Mholanzi amesema wamiliki wa Man United wanafahamu kuwa itakuwa "vigumu sana" kushinda ligi msimu huu.
"Nadhani familia ya Glazer wanafahamu hilo, vinginevyo nisingekubali kuchukua kazi hii," amesema.
Van Gaal alisaini mkataba wa miaka mitatu Old Trafford baada ya kumaliza kukiongoza kikosi cha Uholanzi katika Kombe la Dunia.
Alishinda ligi katika msimu wa kwanza akiwa Barcelona na Bayern Munich, lakini anaamini meneja yoyote anatakiwa kutazamwa katika msimu wa pili.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...