welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Thursday, 14 August 2014

YANGA YAFANYA USAJILI MPYA..... USAJILI KIMYA KIMYA - JEMBE JIPYA

Napenda kuwataarifu tumesajili beki wa kushoto mpya na chipukizi kutoka JKT Ruvu kwa jina la Edward Charles na tumeshakamilisha taratibu zote za usajili wake na kumsainisha Mkataba wa miaka mitatu.
Kikosi chetu cha siri cha usajili kikiongozwa na Francis Kifukwe kimefanikisha kazi hiyo leo baada ya kukutana na uongozi wa JKT.
Ni moja ya pendekezo la kocha Maximo, na huyu kijana ni kati ya chipukizi waliopo timu ya taifa ya wakubwa kwa sasa, Taifa Stars chini ya kocha Mholanzi, Mart Nooij ambao wanainukia vizuri.
Ni mkabaji mzuri, ana nguvu, kasi - mbinu za anapokuwa na mpira na asipokuwa nao na pia hupanda vizuri kushambulia na kurudi kwa haraka. Anasifika kwa kupiga krosi nzuri pamoja na mpira iliyokufa.

Edward Charles

2 comments:

  1. noumaaa saaana

    ReplyDelete
  2. naikubali yanga jamani uwii,,,,hapo nazidi kuwapenda bure

    ReplyDelete

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...