Katika
hali ya kushangaza, mtu mmoja anayefahamika kwa jina la Ali, mkazi wa
Mwananyamala jijini Dar, amekamatwa na polisi baada ya kudaiwa
kuunganisha visivyo halali, mitambo ambayo iliwawezesha watu kuangalia
matangazo ya televisheni ya vituo mbalimbali kwa malipo rahisi.Awali,
msamaria mwema mmoja alipiga simu kwa kikosi kazi cha Operesheni Fichua
Maovu (OFM) cha Global Publishers na kukitonya juu ya uwezo wa mtu huyo
anayewashangaza kwa utaalamu wake wa kuunganisha mitambo hiyo bila
kugundulika.
“Hapa
kuna watu kama 80 hivi wameunganishwa, wanaangalia televisheni za Azam,
Zuku na nyingine kwa bei chee, lakini wanaangalia mipira, filamu na
kila kitu, yaani huwezi kuamini kaka,” chanzo hicho kilinyetisha kwa
OFM.Katika
kujiridhisha, kikosi kazi chini ya kamanda mkuu, kilitembelea eneo la
tukio na kufanya ukaguzi wa siri, uliothibitisha kuwepo kwa huduma hiyo,
lakini bila ya kuwepo kwa dekoda za vituo hivyo vya televisheni
vinavyotolewa kwa malipo.Baada
ya kujiridhisha huko, OFM ilifanya mawasiliano na wahusika wa vituo
hivyo, ambao nao walitembelea eneo hilo la tukio na kujionea wenyewe.
Wahusika hao walikuwa ni Afisa Leseni wa DSTV na Afisa Mauzo wa Azam Tv
pamoja na mtu mmoja kutoka chama cha hakimiliki cha COSOTA.OFM
iliwashauri maofisa hao kuripoti jambo hilo kituo cha polisi, ushauri
ambao waliukubali na kwenda kutoa taarifa Kituo cha Polisi Oystebay
ambao waliongozana na watu hao hadi Mwananyamala.Kufika
nyumbani kwa mtuhumiwa huyo ambaye pia ni maarufu kwa jina la utani
kama Masetelaiti, Polisi walifanikiwa kumkamata na baada ya upekuzi,
waligundua kuwepo kwa mitambo ya aina mbalimbali, vikiwemo ving’amuzi
vya aina mbalimbali, modulators, Receivers na vifaa vingine vikionekana
vikiwa vimeunganishwa kwa utaalamu wa hali ya juu katika ukuta wa sebule
yake.
Afisa Leseni kutoka Cosota, Zephania Lyamuya alisema jamaa huyo
anastahili kupelekwa Polisi kutoa maelezo kwani licha ya kutokuwa na
leseni ya kufanya biashara hiyo, pia amekuwa akiwanyonya waigizaji
wanaostahili kulipwa kila filamu zao zinaporushwa katika televisheni za
nje.Naye
Afisa Mkuu wa Mauzo kutoka kampuni ya Azam aliyejitambulisha kwa jina
la Shah Seffu (pichani kulia), alisema kuwa operesheni hiyo ni moja kati
ya hatua walizozipanga kumaliza tatizo la kuingilia mawasiliano ya
televisheni jambo ambalo limeonekana kukua kwa kasi nchini.Baada
ya kuvikusanya vifaa hivyo vilipelekwa katika Kituo cha Polisi cha
Oysterbay sambamba na mtuhumiwa kutoa maelezo ambapo jalada
lilifunguliwa OB/RB/16106/2014, KUINGILIA MAWASILIANO YA TELEVISHENI
SOURCE:GLOBAL PUBLISHER
No comments:
Post a Comment