Staa wa filamu Bongo, Lucy Komba.
Sherehe hiyo ilifanyika mwishoni mwa wiki iliyopita katika Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Posta jijini Dar ambapo mbali na watu wa kawaida,
wake wa viongozi mbalimbali nchini pamoja na baadhi ya wasanii wa Bongo
Movies walihudhuria.Miongoni mwa matukio ambayo yaliibua
mshangao kwa waalikwa ni bibi harusi mtarajiwa (Lucy) kutinga ukumbini
hapo akiwa ndani ya baiskeli yenye magurudumu matatu (guta) akiwa na
wapambe wake ambao walikuwa peku miguuni. Kwenye guta hilo
lililotengenezewa kibanda cha asili kilichowekwa nyasi juu, Lucy alikaa
ndani yake huku wapambe wake wakiwa wameshika nyungo ndogo kuashiria
asili ya Mtanzania.“Ama kweli hii ni ya
aina yake, hebu angalia nguo yake alivyoitengeneza kwa kweli inavutia
sana, full utamaduni,” alisikika mmoja wa watu walioudhuria sherehe
hiyo.Ulipofika wakati wa kufungua shampeni, nayo ilikuwa ya aina yake. Aliandaliwa pombe ya kienyeji ya mkoani Ruvuma ijulikanayo kama Kangara ambayo aliiweka ndani ya kibuyu kidogo huku akipita kugongesha na wageni waalikwa.
Akiingia ukumbini kwa mbwembwe.
Baadhi ya marafiki zake waliotoka nchi mbalimbali akiwemo muigizaji
kutoka nchini Italia, Angela Howell, alidondosha chozi la furaha
alipoona waalikwa wanakula ndafu badala ya keki kama ilivyozoeleka na
wengi.
Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye kuangusha nyingine Denmark.
Lucy Komba anatarajia kufunga ndoa hivi karibuni na mchumba wake aitwaye Stanley, raia wa Denmark. Watafanya sherehe kubwa Bongo na baadaye kuangusha nyingine Denmark.
No comments:
Post a Comment