Stori ambazo huwa zinakuwepo mtaani zikihusisha maisha ya eneo fulani
hutufanya wengi kuvutiwa na simulizi hizo na kutamani kufahamu hata
kidogo undani wa hizo habari zinazosemwa.
Iringa ni mkoa ambao una sifa inayosimamishwa na Mtemi Mkwawa
aliyekua chifu na kiongozi mkuu wakati wa upanuzi wa ukoloni wa
Ujerumani mwishoni mwa karne ya 19 Iringa.
Ukubwa wa jina Gangi lilonga linatokana na Jiwe linalopatikana
Manispaa ya Iringa eneo la Gangi Lilonga ambalo kulingana na historia ya
eneo hilo na simulizi za jiwe hilo ambalo linasemekana lilikuwa
likiongea alikua akilitumia sana Mtemi Mkwawa.
Kwa miaka ya hivi karibuni jiwe hili halitumiki tena kwa imani hizi
na kwa sasa limefanywa kama kivutio kwa watalii mbalimbali ambao
wanafika kulishangaa,mambo ya Digital kwa sasa wanasema kuwa hakukua na
sauti hizo za ajabu.
Kutokana na sehemu yenyewe kuwa mlimani inasemekana kuwa wazee
walikua wanashindwa kujua kama ile ni Echo Sound yaani Mwangwi hivyo mtu
anaweza kuongea kutoka mbali ukahisi jiwe ndilo linalozungumza.
Tafsiri ya jina hili Gangi Lilonga maana yake GANGI(jiwe)
LILONGA(linaloongea),Mzee Macha ni mwenyeji kidogo Mkoa wa Iringa uwepo
wake zaidi ya miaka 30 anashare na sisi anayoyajua kuhusu jiwe hili
No comments:
Post a Comment