MTOTO
Regina Geofrey (miezi 14), ameuawa kwa kunyongwa na baba yake mzazi
Geofrey Kilingwa ‘Simbaiwe’ (27), kwa madai alizaliwa akiwa ametanguliza
makalio yake.
Baba wa binti huyo ambaye pia ni mganga wa kienyeji anayeishi kitongoji
cha Mwikang’ombe, Kijiji cha Katuma, Mpanda, alitenda unyama huo kwa
madai mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio ni mkosi na nuksi kubwa
katika shughuli zake hizo za uganga wa kienyeji.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Katavi, Dhahiri Kidavashari, aliwaambia
waandishi wa habari jana kuwa, mzazi huyo aliyetenda uhalifu huo Julai
20 mwaka huu ambako alikamatwa na Jeshi la Polisi Agosti 26 mwaka huu.
Inadaiwa kuwa, siku hiyo ya tukio, mtuhumiwa baada ya kumnyonga hadi
kufa binti yake huyo, alimzika kwa siri katika kibanda chake
anachofanyia shughuli zake za uganga wa kienyeji.
Akisimulia mkasa huo, Kamanda Kidavashari alidai kuwa, mtoto Regina
alikuwa anasumbuliwa na ugonjwa ambao haukufahamika kwa zaidi ya mwezi
mmoja, ndipo Simbaiwe alipolazimika kuanza kumuuguza kwa siri pasipo
mkewe kufahamu, kwani alimdanganya amepelekwa kutibiwa na babu yake
huko Mwanza.
Inaelezwa kuwa, kibanda anachofanyia kazi zake za uganga kiko mbali na
makazi yake, hivyo ilikuwa rahisi kumficha mtoto wake huyo kwa zaidi ya
mwezi mzima akimtibu bila mkewe kufahamu.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, wakazi wa kitongoji cha Mwikan’gombe
wakiongozwa na Mwenyekiti wao, walimtilia shaka mtuhumiwa kutokana na
tetesi zilizozagaa eneo hilo kuwa mtoto Regina alikuwa ameuawa na baba
yake mzazi na kuzikwa kwa siri.
Inadaiwa wakazi hao na Mwenyekiti wao, walifika nyumbani kwa mtuhumiwa
na kuhoji alipo binti yake ambako alipinga vikali, lakini alipopekuliwa
kibandani kwake, walibaini kuweko kwa tuta dogo lililokuwa limechimbwa
siku za karibuni.
Kidavashari, aliongeza kuwa wakazi hao waliamua kufukua tuta hilo na kukuta kichwa cha mtoto huyo ndipo wakaitaarifu polisi .
Mama ya marehemu, Maria Exavery (22), alidai kuwa hakuhusishwa wala kupewa taarifa kwamba binti yake huyo amekufa.
“Mie nilikuwa nafahamu kuwa, Regina yuko kwa babu yake Mwanza akitibiwa,” alisema Maria.
Naye Regina Kaboni (40), mkazi wa Isamilo Mwanza, ambaye alikuwa
akitibiwa na mtuhumiwa, anadai kuwa alishirikishwa katika maziko ya
binti huyo.
“Hata hivyo…nilistushwa sana kwa kitendo cha mtuhumiwa kumzika mwanaye
bila ya kumshirikisha mkewe, nilipomuuliza alidai kuwa kwa mila ya kwao,
mtoto aliyezaliwa kwa kutanguliza makalio, mama mzazi wa mtoto ni mwiko
kushirikishwa katika maziko ya mtoto huyo,” alidai.
Kwa mujibu wa Kamanda Kidavashari, watu wanne wakiwemo wazazi wa
marehemu wanashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano zaidi na
watafikishwa mahakamani mara tu baada ya upelelezi wa awali kukamilika.
Wengine wanaoshikiliwa na Polisi ni Regina Kaboni ni Msolwa Jacob (29), mkazi wa kitongoji cha Mwikang’ombe.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!
Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com ! Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...
-
UTANGULIZI. Uyoga ni aina ya nyuzi kuvu (fungus) yenye kutofautiana na mimea mingine kwa kukosa chembe chembe zinazowezesha mimea ku...
-
Kutoka Jiji la Chicago Nchini Marekani Kijana wa Kiume Micah ambaye ni msanii wa R&B anayechipukia mwenye umri wa miaka 20 amechuk...
No comments:
Post a Comment