welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Thursday, 4 September 2014

Mtangazaji wa TV Piers Morgan ameacha kazi katika shirika la habari la Marekani la CNN,

Mtangazaji wa TV Piers Morgan ameacha kazi katika shirika la habari la Marekani la CNN, licha ya kupewa nafasi ya kuongeza mkataba wake.
Morgan ame tweet akisema anakwenda "kujaribu mambo mengine mapya" baada ya wakuu wa kituo hicho kumtaka asalie kwa miaka miwili zaidi. Mkataba mpya ungempa nafasi ya kuwa na mahojiano maalum ya vipindi 40.
Piers Morgan alimrithi Larry King, katika kipindi cha mahojiano, lakini kipindi hicho kilifutwa mwezi Machi kufuatia kupoteza umaarufu.
Kipindi kilianzishwa Januari 2011 kikiwa na watazamaji karibu milioni moja, lakini idadi hiyo ilipungua hadi kufikia 270,000.
"Nimekuwa na wakati mzuri katika kipindi cha miaka minne nikiwa na CNN, na nina mheshimu sana Jeff [Zuckerberg, mkuu wa CNN] pamoja na watu wote wanaofanya kazi hapo." Amesema Morgan.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...