
Kocha
Mkuu wa Young Africans Marcio Maximo (kushoto) akiongea na waandishi wa
habari juu ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Big Bullets kutoka Malawi
siku ya jumapili, kulia ni Afisa Habari wa timu hiyo Bw Baraka Kizuguto
Timu
ya Young Africans itashuka dimba la Uwanja wa Taifa jijini Dar es
salaam siku ya jumapili kucheza mchezo wake wa mwisho wa kirafiki wa
kimataifa dhidi ya timu ya Big Bullets FC (zamani Bata Bullets)
inayoshiriki Ligi Kuu ya TNM nchini Malawi.Young Africans ambayo
imeshacheza michezo minne mpaka sasa ya kirafiki ukiwemo mmoja wa
kimataifa katikati ya wiki hii dhidi ya timu ya Thika United kutoka
nchini Kenya imeshinda michezo yote.Akiongea na waandishi wa habari leo
katika mkutano na waandishi wa habari, kocha mkuu wa Young Africans
mbrazil Marcio Maximo amesema mchezo huo wa siku ya jumapili utakua ni
kipimo kizuri kwa vijana wake kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya Vodacom
wiki mbili zijazo.
"Mchezo
uliopita tuliocheza dhidi ya Thika United ulikua ni mchezo mzuri,
tumepata nafasi ya kuyaona mapungufu yetu na kama mnavyofaham wenzetu
wako katika Ligi inayondelea hivyo walicheza kitimu zaidi kuliko sisi na
hata Big Bullets FC pia namini kitakua ni kipimo kizuri kwetu " alisema
Maximo".
Kuhusu
timu ilivyocheza Maximo amesema hapendi kumzungumzia mchezaji mmoja
mmoja, na masula ya uchezaji hapendi kuyaongea kwa jamii, hiyvo yeye
kama kocha alishaongea na wachezaji na kuwaelezea mapungufu
yaliyojitokea na kipi wanapaswa kukifanya katika michezo inayofuata.
Aidha
Maximo aliongeza kuwa yeye kwa sasa hana kikosi cha kwanza, hana
mchezaji mwenye uhakika wa namba, kilichopo kwake ni kundi la wachezaji
ambao wote wana nafasi ya kucheza kulingana na mahitaji ya mchezo
wenyewe.
Afisa
Habari wa Young Africans Bw Baraka Kizuguto amesema taratibu zote za
mchezo zimekamilika na timu ya Big Bullets FC kutoka nchini Malawi
inatarajiwa kuwasili kesho jijini Dar es salaam na kufanya mazoezi jioni
katika Uwanja wa Karume eneo la Ilala.
"Mchezo
wa jumapili tunatarajia utakua ni mchezo mzuri, ukizingatia timu ya Big
Bullets FC inashika nafasi ya pili kwenye msimamo wa Ligi Kuu nchini
Malawi iiliyofikia mzunguko wa 17 kwa tofauti ya pointi moja na vinara,
na kocha Maximo alipendekeza tupate timu tofauti kutoka ukanda wa Kusini
mwa Afrika baada ya kuwa tayari tumeshacheza na timu ya Ukanda wa
Afrika Mashariki" alisema Kizuguto.
Siku
ya jumapili mechi inatarijiwa kuanza majira ya saa 10 kwa saa za Afrika
Mashariki na viingilio vya mchezo ni kama ifuatavyo:
VIP A Tshs 30,000/=
VIP B & C Tshs 20,000/=
Orange Tshs 10,000/=
Blue & Green Tshs 5,000/=
No comments:
Post a Comment