Mwanamume mmoja mjini Los Angeles
nchini Marekani, amefungwa jela mwaka mmoja baada ya kupatikana na hatia
ya kusambaza picha za utupu wa mchumba wake kama hatua ya kulipiza
kisasi.
Yeye ni mtu wa kwanza kuhukumiwa chini ya sheria
inayojulikana kama 'Revenge porn' yaani wanaopatikana na hatia ya
kulipiza kisasi kwa kusambaza picha za wapenzi wao wa zamani wakiwa
uchi.
Noe Iniguez, mwenye umri wa miaka 36, alipatikana na hatia
ya makosa matatu ya uhalifu ikiwemo kusambaza picha za mpenzi wake
kinyume na sheria pamoja na kuiuka agizo la mahakama la kumzuia
kumkaribia mpenzi wake wa zamani.
Iniguez alitumia jina bandia
kutuma ujumbe wa kumchafulia jina mpenzi wake kwenye ukurasa wa Facebook
wa mwajiri wake, mwezi Disemba 2013. Yote haya kwa sababu tu mwanamke
huyo aliachana naye.
Mnamo mwezi Machi, alisambaza picha ya
mpenzi wake akiwa nusu uchi huku akimtusi na kusema ni mlevi na pia
kumtaka mwajiri wake kumfuta kazi.
Chini ya sheria ya jimbo la
Carlifonia iliyopitishwa mwaka 2013, ni kinyume na sheria kusambaza
picha za mtu yeyote akiwa uchi kwenye mitandao ya kijamii na
kumsababishia shinikizo la mawazo mtu yule.
Jaji David Fields alimhukumu, Iniguez mwaka mmoj
No comments:
Post a Comment