
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya amesema
kuwa Kenya haitachoka katika vita vyake dhidi ya ugaidi kufuatia
shambulizi lililofanywa dhidi ya wachimba migodi mjini Mandera Kaskazini
ya Kenya.
Ametoa kauli hiyo katika hotuba yake kwa taifa baada ya
shambulizi lengine lililofanywa na kundi la wanamgambo la Al Shabaab
dhidi ya wakenya wasiokuwa na hatia.
Kundi hilo liliwavamia wachimba migodi 36 waliokuwa katika machimbo ya kokoto mjini Mandera.
Kundi hilo liliwaua wakenya wengine 28 waliokuwa wanasafiri kutoka mjini Mandera siku kumi zilizopita.
Kenyatta
amelaani wanamgambo hao wa Al Shabaab kwa kutaka kuigawanya Kenya
katika msingi ya kidini na kuwataka wakenya kuungana dhidi ya kile
alichokitaja vita dhidi ya ugaidi.
Kenyatta aliwataka magaidi wa Al Shabaab kama wanyama walio na kichaa.
Aliwasihi wakenya kuungana katika vita dhidi ya magaidi.
Siku
kumi zilizopita, Al Shabaab waliuwaua abiria 28 waliokuwa wanasafiri
kwa basi kutoka mjini Mandera karibu na mpaka na Somalia kuelekea
likizoni makwao. Wengi wa waliouawa walikuwa walimu wa shukle za umma.
No comments:
Post a Comment