![]() |
Paul anapenda sana kujihusisha na maswala ya wanyama hasa Nyoka |
Watu nchini Marekani wameelezea
ghadhabu na hasira zao kwenye mitandao ya kijamii kufuatia utafiti wa
mtaalamu wa wanyamapori Paul Roslie kumezwa na Nyoka aina ya Anaconda
ili ku chunguza maumbile ya ndani ya Nyoka huyo.
Lengo la utafiti
huo ambao ulikuwa wa kwanza wa aina yake duniani, ilikuwa ni kuchunguza
maumbulie ya ndani ya Nyoka huyo anayepatikana katika msitu wa Amazon.
Hata hivyo inaarifiwa bwana Paul alilazimika kusitisha utafiti wake ambao umezua utata muda mfupi tu baada ya kuuanzisha.
Watu
nchini Marekani walijionea kwenye televisheni zao kipindi kilichokuwa
kinapeperushwa cha mtaalamu huyo kuingia ndani ya tumbo la Anaconda
akiwa amevalia vazi maalum ambalo yangesaidia kuchunguza kiwango cha
joto mwilini mwake na pia kupima mipigo ya Moyo wake wakati akiwa ndani
ya tumbo la Nyoka huyo.
Rosolie na kikundi cha wasaidizi wake walipata Nyoka ya Anaconda
mwenye uzito wa kilo 180, walipokuwa katika msitu huo. Alipanga kuwa
ataonyeshwa kwenye stesheni hio akiwa anamezwa mzima mzima na Nyoka
huyo.
Rosolie alionekana akiingia ndani ya mdomo wa Anaconda kwa kichwa chake huku wenzake wakimtazama.
Alikuwa amevalia vazi maalum lenye Carbon na likiwa limepakwa damu ya Nguruwe, kabla ya kujielkeza kwa Nyoka huyo kama mlo wake.
"sikutana kumhangaisha mno mnyama na pia mimi mwenyewe sikutaka kujiumiza. ''Paul anapenda sana kujihusisha na maswala ya wanyama hasa Nyoka
"nilitaka kuhakikisha kuwa vazi langu halitamjeruhi Nyoka huyo kwa vyovyote vile.''
''Mimi
mwenyewe sikuogopa hata kidogo. Watalaamu walifanyia jaribio vazi
langu, kwa hivyo tulijua kuwa halitamwathiri kwa vyovyote Nyoka huyo. ''
Lakini
baada tu ya saa moja ya mtaalamu kuingia ndani ya tumbo la Nyoka na
kuanza kubanwa, aliamua kusitisha utafiti wake akihofia kuwa angeumizwa
na Nyoka huyo mkubwa. Alisikika akiwaita wenzake kwa kifaa maalum cha
kupaza sauti kilichokuwa kimewekwa kwenye vazi lake na kuwamabia kuwa
anaumizwa.
''Nahisi kama mifupa yangu inasagwa sagwa, njooni mniondoe hapa.'' alisema Paul.
Namna
ambavyo Rosolie aliponea kufa baada ya kubanwa na Nyoka huyo bado ni
muujiza ingawa aliweza kupata hewa kutokaa kwa vazi lake hilo kwa saa
tatu.
SOURCE:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment