![]() |
KABURI NA GARI ALILOZIKWA NALO MAITI |
Katika siku za hivi karibuni picha
za mtu ambaye alizikwa ndani ya gari aina ya Hummer SUV Jeep nchini
Nigeria zimekuwa zikienea katika mitandao ya kijamii na kuzua mjadala
miongoni mwa raia wengi wa taifa hilo.
Picha hizo zilitoka katika mtandao wa twitter wa msichana mmoja raia wa Kenya anayetumia jina @Sankorie.
Alielezea
kushangazwa na kusema kuwa wanaume wa Nigeria ni matajiri hadi wengine
huzikwa ndani ya magari yenye thamani ya juu,swala ambalo haliwezi
kufanyika nchini Kenya.
Je, unadhani ni kweli kwamba mtu anaweza kuzikwa ndani ya gari lake?
No comments:
Post a Comment