
Shirika la habari la Uingereza BBC limemtaja nyota wa timu ya taifa
ya Algeria Yacine Brahimi kuwa mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2014
ambapo Brahimi ambaye anachezea klabu ya Ureno ya Fc Porto anakuwa raia
wa kwanza wa Algeria kutwaa tuzo hiyo ambayo hutolewa na BBC kila mwaka.
Brahimi ametwaa tuzo hii kufuatia uwezo aliouonyesha mwaka huu akiwa
na timu yake ya taifa hasa kwenye michuano ya kombe la dunia ambako
Algeria walifanikiwa kufika hatua ya 16 bora.
No comments:
Post a Comment