![]() |
Muimbaji wa
Uganda, Juliana Kanyomozi amefunguka kwa urefu kuhusiana na masuala
mbalimbali kwenye mahojiano aliyofanyiwa na mtandao wa SatisfashionUG. Miongoni mwa mambo aliyohojiwa ni pamoja na kuvuja kwa picha za utupu za muimbaji mwenzie wa Uganda, Desire Luzinda. “Kwanza kabisa katika kesi nyingi kamwe huwa sio kosa la mwanamke,” anasema Juliana.
“Kama
wewe ni mtu mzima na umempenda mtu unajua kuwa hakuna kikomo cha kipi
kitatokea kwenye chumba binafsi cha watu wazima wawili. Kama hautaenda
mbali zaidi kumfurahisha mwanaume wako, atakuacha na kisha utahukumiwa
kwa hilo,” aliongeza.
“Pindi mwanaume anapovunja uaminifu na kuamua kushare vitu hivyo siri kwa dunia nzima na kutumia vyote dhidi ya mwanamke – ndio maana bado tuna safari ndefu kama wanawake kukemea tabia hiyo.”“Nachukizwa na wanaume wa aina hii. Wanatia aibu. Kinachoshangaza zaidi ni kuwa ni wanawake pekee ndio wanaokuwa wahanga kwenye visasi hivi vya mashambulizi ya purn. Unapofanya kitu kama hicho kwa mwanamke, hauwaumizi wanawake wote tu bali pia mama yako, mabinti zako na dada zako.” Juliana alitolea pia mfano wa udukuzi uliofanyika nchini Marekani na kudai kuwa pamoja na picha za wasanii mbalimbali kuvuja hakuna chombo cha habari cha kuaminika kilichozianika. “Inanisikitisha hapa nyumbani, kinyume chake ndio kinatokea.” |
Saturday, 24 January 2015
A BEATIFULLY LADY FROM UGANDA:JULIANA KANYOMOZI
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!
Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com ! Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...
-
UTANGULIZI. Uyoga ni aina ya nyuzi kuvu (fungus) yenye kutofautiana na mimea mingine kwa kukosa chembe chembe zinazowezesha mimea ku...
-
Kutoka Jiji la Chicago Nchini Marekani Kijana wa Kiume Micah ambaye ni msanii wa R&B anayechipukia mwenye umri wa miaka 20 amechuk...
No comments:
Post a Comment