![]() |
ALI KIBA FOR REAL |
Mlinzi wa getini hapo amezungumza na Uheard na Soudy Brown alisema kuwa Ali Kiba alifika getini lakini cha kushangaza hakupita mlangoni aliruka ukuta na kuingia ndani.
‘’Ali Kiba alifika hapa wenzake mimi nilikuwa hapa getini lakini nikashangaa ameruka ukuta’,alisema mlinzi huyo.
Hata hivyo haikuishia hapo habari zinasema kuwa Ali Kiba alishindwa kumpa mkono msanii mwenzake Mwana Fa huku baunsa wake akimzuia msanii huyo kumsalimia Ali Kiba.
Katika tamasha hilo mashabiki wa mastaa wawili Ali Kiba na Diamond Platinumz walifanya vurugu kwa kurusha chupa za maji baada ya wasanii hao walivyokuwa wakipanda jukwaani kupafomu.
Hata hivyo Ali Kiba akizungumzia tukio hilo alisema halikuwa tukio la kishirikina ila alishindwa kupita getini kwa sababu watu walikuwa wengi.
No comments:
Post a Comment