Idara ya polisi ndio taasisi inayochukua hongo zaidi nchini Tanzania kulingana na ripoti ya ufisadi katika jumuiya ya Afrika mashariki.
Ripoti hiyo inasema kuwa maafisa wa polisi walipokea asilimia 25 ya
hongo zote zilizotolewa kwa wafanyikazi wa taasisi za uma mwaka
uliopita.
Ya pili ni idara ya mahakama,ambayo wafanyikazi wake
walitia mfukoni asilimia 18 ya hongo,huku mashirika yalio na majukumu ya
usajili na utoaji wa leseni yakiwa katika nafasi ya tatu kwa asilimia
10.
kwa mujibu wa gazeti la The Citizen, Idara ya Polisi nchini
Tanzania imetajwa kuwa ya tatu kwa ufisadi katika jumuiya ya Afrika
mashariki.
Polisi wa Uganda wanaongoza wakifuatiwa na wale wa Kenya katika nafasi ya pili na wale wa Burundi wakiwa katika nafasi ya nne.
Kulingana na ripoti hiyo maafisa wa polisi wa Rwanda ndio wasiochukua hongo ya juu Afrika mashariki.
Utafiti
huo ulifanywa mwezi Julai na Agosti mwaka uliopita na shirika la lenye
na maslahi ya kimaendeleo barani afrika ForDIA likishirikiana na Jukwaa
la uwazi nchini tanzania Trafo.
SOURCE:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment