welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Saturday, 17 January 2015

INASIKITISHA: WATU WASIOJULIKANA WAFUKUA KABURI NA KUTOKOMEA NA MWILI WA MAREHEMU KUSIKO JULIKANA.

Watu    wasiofahamika  wamefukua kabuli   na kubeba  mwili wa marehemu aliyekuwa amezikwa kwenye makaburi ya Isanjsndugu   Tarafa ya Nsimbo Wilaya ya Mlele  Mkoani Katavi  kwa kile kinachodaiwa kuwa ni imani za  kishirikina
Kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Nsimbo  Michael  Kasanga(CCM) alisema tukio hilo la imani za kishilikina lilitokea hapo juzi kwenye makaburi ya  Isanjandugu  Tarafa ya Nsimbo
Alisema  kabuli la marehemu huyo ambalo lilifukuliwa na  watu wasiojulikana  ililigunduliwa hapo  juzi na wananchi  wawili  waliokuwa  wanakwenda shambani  ambao walipita jirani na makabuli hayo na kuona kabuli hilo limefukuliwa
 Diwani Kasanga alieleza  baada ya wananchi hao wawili  kuona kabuli  hilo  limefukuliwa walishitushwa na hari hiyo  na iliwalazimu kurudi kijijini na kutoa taarifa  kwa uongozi wa serikali ya kijiji
 Alisema baada ya  viongozi wa Kijiji hicho kupata taarifa hiyo waliongozana  na baadhi ya wananchi  kwenda kwenye maeneo hayo ya mababuri ya Kijiji  hicho
 Baada ya kufika kwenye eneo hilo la kabuli hilo  walikuta  limefukuliwa na watu ambao hawejafamika  huku  mabaki ya mwili wa marehemu huyo   yakiwa yamebebwa  kwa kile kinachoonekana  ni imani za kishirikina
 Alisema   kabuli hilo  lilishindwa kufahamika jina la marehemu  aliyekuwa amezikwa kwenye kabuli hilo kutonana na kile  kilichoonekana kuwa kabuli hilo lilikuwa ni la muda mrefu
 Diwani Kasanga alifafanua kuwa imekuwa ni tabia  ya muda mrefu kwa wananchi wa Kijiji hicho  kuwa  na tabia ya  kwenda kwenye makabuli hayo mida ya usiku na kuoga dawa za kienyeji juu ya makabuli kwa imani za kishilikina  
 Alisema  anatowa wito kwa wananchi wa Kijiji hicho kuacha tabia hiyo ya kuchezea kwenye makabuli  na kuogea dawa kwani tabia hiyo ya imani  potofu  sio  nzuri kwenye jamii

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...