welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Saturday, 10 January 2015

Mmiliki wa Blog apewa adhabu, kifungo miaka kumi jela na viboko 1000…

http://i1.wp.com/millardayo.com/wp-content/uploads/2015/01/548x331_raif_0.jpg 
Mmiliki wa Blog moja Saudi Arabia amehukumiwa kifungo na kuchapwa viboko hadharani kwa kukutwa na hatia ya kuandika habari katika tovuti yake iliyodaiwa kuitukana Dini ya Kiislamu pamoja na kushinikiza wananchi wa nchi hiyo kukataa utawala wa kidini.
Raif Badawi ambaye ni mwanzilishi wa Blog hiyo inayoitwa Liberal Saudi Network amehukumiwa kifungo cha miaka 10 jela na kuchapwa viboko 1000 hadharani, ambapo kila wiki atakuwa akichapwa viboko 50.
Watu katika mitandao ya kijamii na waharakati wameandika ujumbe wa kuchukizwa kuhusiana na hukumu aliyopewa Blogger huyo kwa kuandika ujumbe wenye hashtags “#FreeRaif, #IStandWithRaif na #JeSuisRaif.
Mbali na hukumu hiyo, Badawi aliamriwa pia kulipia faini ya dola 226,000 huku mwanasheria wake akihukumiwa miaka 15 jela kwa makosa mbalimbali.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...