Mshindi wa mbio za Boston na Chicago
Marathon katika kipindi cha miaka miwili iliopita mkenya Rita Jeptoo
amepigwa marufuku katika mchezo huo kwa miaka miwili baada ya
kugunduliwa alitumia dawa za kusisimua misuli,shirikisho la riadha
nchini Kenya AK limesema.
''AK imefuata maagizo yote katika kisa
cha Rita na kwamba ni haki kwa yeye kupewa marufuku ya miaka
miwili'',afisa mkuu wa shirikisho hilo Issac Kamande aliwaambia
waandishi habari.Jeptoo amekana kutumia dawa za kusisimua misuli ,akiwaamba wana habari mwaka uliopita kwamba madai hayo dhidi yake ni ya uongo.
chanzo BBC-SWAHILI
No comments:
Post a Comment