welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Friday, 30 January 2015

NMB imesogeza huduma hii kwenye Kikao cha Makamishna wa Polisi Dodoma

1
Meneja Mwandamizi katika kitengo cha wateja binafsi Suzan Shuma akimjazia fomu Kamishna wa Polisi kutoka makao makuu ya jeshi la Polisi, Paul Chagonja, fomu itamrahisishia kupata taarifa fupi za akaunti yake ya NMB kupitia mtandao wa E-mail (E-statement).
3
Kamishna wa Polisi Paul Chagonja, Kamanda Thobias Angengeye pamoja na Meneja Mwandamizi katika kitengo cha wateja binafsi, Suzan Shuma. kwenye banda la Huduma za NMB Dodoma
Kikao cha Makamishna wa Jeshi la Polisi kinachofanyika Dodoma leo kinafikia mwisho, tuliona jinsi ambavyo Benki ya NMB ilikuwa nao bega kwa bega kuanzia siku ya kwanza Kikao hicho kilipoanza siku ya Jumatatu January 26.
Mbali na ufadhili uliofanywa na Benki hiyo kutoa mil. 75 kwa ajili ya kikao hicho, NMB ilikuwa ikitoa huduma mbalimbali katika mabanda yaliyowekwa nje ya ukumbi wa St. Gaspar, Dodoma.
Moja ya huduma ambazo zilitolewa katika mabanda hayo ni kutoa na kuweka fedha kupitia NMB wakala ambapo kupitia teknolojia ya Max Malipo, mteja anaweza kutoa na kuweka fedha na pia kupata huduma zingine za kibenki ambazo angeweza kuzipata katika tawi lolote la NMB hivyo walijionea jinsi ambavyo huduma hiyo imerahisisha huduma za NMB karibu nao.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...