Maafisa wa polisi nchini Kenya
wameupata mwili wa shahidi muhimu wa mahakama ya ICC siku chache tu
kabla ya kutoa ushahidi wake katika kesi ya naibu wa rais katika
mahakama hiyo.
Ripoti za vyombo vya habari nchini Kenya zinasema
kuwa mwili wa Meshash Yebei ulipatikana karibu na mto zaidi ya wiki moja
baada ya kuonekana akibebwa na kuingizwa katika gari moja lisilo na
nambari za usajili katika mji wa Eldoret,umbali wa kilomita 200.
Bwana
Yebei alitarajiwa kusafiri kuelekea mjini Hague kwa kesi dhidi ya bwana
Ruto-makamu wa rais ambaye anakabiliwa na mashtaka yanayohusiana na
mashambulizi dhidi ya watu wa jamii ya kikuyu katika makaazi ya
wakalenjin huko Rift valley wakati wa ghasia za baada ya uchaguzi miaka
saba iliopita.
chanzo:BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment