Katika
kutekeleza sera ya Matokeo makubwa sasa (BRN), shule ya Sekondari ya
Naliendele iliyopo katika manispaa ya Mtwara mikindani imepokea mzigo wa
kutosha wa vitabu vya masomo ya Sayansi. Vitabu hivyo vimetolewa na
serikali ikishirikiana na wahisani wake ambapo lengo ni kuhakikisha
kitabu kimoja kinatumiwa na wanafunzi wawili. Wakizungumzia tukio hili
baadhi ya waalimu wa shule hiyo wamefurahishwa na mgao huo wa vitabu na
kuomba kuletewa vingine vingi vya masomo ya sanaa na sayansi ya jamii.
 |
Mwalimu Kajuta Zongo (Katibu no 1 wa shule) Akiwa haamini kilicho tokea |
 |
Baadhi ya vitabu vilivyo pokelewa tayari kwa kusajiliwa na kuanza kutumika. |
No comments:
Post a Comment