
Wakati idadi kubwa ya watu duniani ikiendelea kupinga mapenzi ya jinsia moja ambayo yamehalalishwa na baadhi ya nchi kubwa duniani, Russia limetolea hili jingine jipya.
Ni habari ambayo imezungumziwa sana kwa saa kadhaa zilizopita baada ya Wanawake wawili ambao ni wapenzi wa jinsia moja kupiga picha mbele ya Mwanasiasa maarufu kwa kupinga mapenzi ya jinsia moja.
Wanawake hawa walijikuta kwenye ndege moja na Mwanasiasa huyo wakitokea Moscow kwenda St. Petersburg ambapo waliamua kupiga picha ya selfie wakipigana busu huku Mwanasiasa akionekana nyuma yao.
Waliipost picha baadae na kuandika ‘Sisi tunafuraha, yeye hawezi kuwa nayo… lakini kwani nani anajali?’ Milonov hakusema chochote baada ya kugundua tunapiga picha ila alijificha’
No comments:
Post a Comment