![]() |
Raisi Uhuru Kenyata na Jaguar |
Rais
wa Kenya, Uhuru Kenyatta, amemteua Jaguar kuingia kwenye bodi ya
mamlaka NACADA inayohusika na kampeni dhidi ya matumizi ya pombe na dawa
za kulevya ya nchini humo.
Jaguar
amechaguliwa katika nafasi hiyo na maafisa wengine 302 kutokana na
hekima, uzoefu, ujuzi, nguvu, ubunifu na kusaidia kundi la vijana katika
jamii.
Uteuzi huo ulitangazwa kupitia tangazo gazetini April 27.
Hata hivyo wengi wanahisi Jaguar amepewa shavu hilo kutokana na ukaribu na urafiki mkubwa alionao na Uhuru Kenyatta.
No comments:
Post a Comment