Rafiki_wa_msichana. Kuna makosa mengine tunafanya kwa sababu tu ya
kukosa maarifa katika maeneo fulani. Kuna fursa zimetupita kwa sababu ya
upeo mdogo tulionao. Usiri mkubwa wa kujadili baadhi ya mambo katika
ngazi ya familia umesababisha madhara ambayo yangeweza kuepukika. Ni
wazazi wachache sana hukaa na mabinti zao na kuwafundisha kwa undani
mambo yanayowahusu, changamoto na jinsi ya kukabiliana na mabadiliko
mbalimbali.Ni wakati sasa wa kutoona haya na kuchukua hatua madhubuti
za kuwasaidia watoto wetu, wadogo zetu, rafiki zetu, n.k Kujitambua,
kujithamini na kuwa na ujasiri wa kutosha kuisimamia kweli.
#mtaijua_kweli_na_hiyo_kweli_itawaweka_huru,
#NENO_lake_ndiyo_kweli
#NENO_lake_ndiyo_kweli

No comments:
Post a Comment