welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Friday, 29 August 2014

FROLA MBASHA ASEMA UJAUZITO ALIONAO NI WA EMMANUEL MBASHA NA SIO GWAJIMA

Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania Flora Mbasha akichat Live katika ukurasa wa Facebook wa EATV 
 Muimbaji wa nyimbo za Injili Tanzania ambae pia ni Mke wa Emmanuel Mbasha amefunguka na kusema kuwa hana mahusiano yoyote ya kimapenzi na na Mchungaji wa Kanisa la kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima,Flora amesema hayo  alipokuwa akichat Live kupitia ukurasa wa Facebook wa EATV katika kipengele cha Kikaangoni Live .Flora amesema kuwa hawezi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mtu ambae ni ndugu yake hivyo Mchungaji Gwajima ni mjomba wake na si mpenzi wake kama ambavyo watu wamekuwa wakizusha kwa lengo la kumchafua na kumshushia hadhi."Hayo ni maneno tu ya watu mtaani ila MchungajiGwajima ni mtumishi wa Mungu na ni uncle wangu ninawezaje kuwa na mahusiano na uncle wangu..? "Alihoji Flora. wakati akijibu ya maswali ya mashabiki ambayo mengi yao yalikuwa yakimtuhumu na huku watu wengi wakitaka kujua ukweli juu ya ugomvi uliopo kati yake na Mumeo kama ni kweli au ni skendo tu za magazeti,Flora aliweka wazi kuwa kuna vyombo vya habari ambavyo vimekuwa na lengo la kumchafua na kumualibia sifa ndio maana walitumia gharama kubwa kufanya wanavyoweza ili kutimiza malengo yao,mbasha amedai kuwa alimua kukaa kimya kwa kuwa hakukuwa na ukweli wowote.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...