Ndege ya shirika la ndege ya malaysia
.Ofisa
mmoja mwanamke mwenye cheo cha juu katika bank kubwa iliyoko mjini
Kuala Lumpur , Malaysia pamoja na mumewe wameshtakiwa kwa kuiba
mamilioni ya dola za kimarekani kutoka katika account za abiria na
wafanyakazi wa ndege iliyopotea ya Malaysia Air Line MH370 ambayo
ilipotea katika mazingira ya kutatanisha,katika bahari ya Hindi mapema
mwezi March.
Pamoja na
kushtakiwa huko, mtu na mkewe hao waliepuka makosa mengine yapatayo 16
kati ya makosa hayo yamo wizi,kukaidi amri ya mahakama na makosa
mengineyo.
Ofisa huyo Nur Shila Kanan anatuhumiwa kutumia cheo chake vibaya katika benki ya HSBC nchini Malaysia kwa kupoka pesa.
Mwendesha
mashtaka aliiambia mahakama moja mjini Kuala Lumpur,Malaysia kwamba
wawili hao walifanikiwa kukwapua dola za kimarekani elfu thelathini
kutoka katika account tatu tofauti za abiria waliopotea na account moja
ni ya mfanyakazi wa shirika hilo la Malaysia Air Line.
No comments:
Post a Comment