![]() |
William Pooley anayetibiwa mjini London, baada ya kupata maambukizo ya Ebola, anatunzwa vizuri |
Familia ya muuguzi huyo wa kujitolea, aliyesafirishwa mjini London,
baada ya kuambukizwa ugonjwa wa Ebola nchini Sierra Leone, wamesema
amekuwa akipata matunzo yaliyo bora
Willliam Pooley mwenye umri wa miaka 29 alirudi nchini Uingereza siku ya
Jumapili na amewekwa kwenye kitengo maalumu katika hospitali ya Royal
Free
Bwana Pooley ambaye alikuwa amejitolea kuwahudumia wagonjwa wa mlipuko
wa Ebola barani Afrika ambao umeuwa watu 1,500 ametajwa kama shujaa na
taasisi moja ya hisani inayojulikana kama Shepherd Hospice aliyoifanyia
kazi nchini Sierra Leone kwa vile alijua hatari zilizokuwepo lakini
akaamua kusaidia
Bwana Pooley anayetoka karibu na mji wa Woodbridge, katika kaunti ya Suffolk ni Mwingireza wa kwanza kupatikana na virusi vya Ebola katika mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea hivi karibuni.
Bwana Pooley anayetoka karibu na mji wa Woodbridge, katika kaunti ya Suffolk ni Mwingireza wa kwanza kupatikana na virusi vya Ebola katika mlipuko wa ugonjwa huo uliotokea hivi karibuni.
SWALI: KWANINI WAAFRIKA WAFE, MZUNGU MMOJA APONE?
No comments:
Post a Comment