Msemaji wa jeshi la Cameroon Luteini Kanali Didier Badjek
amethibitisha kisa hicho na kusema kuwa wamepokonywa silaha na sasa
wamewekwa katika shule
Mapigano hayo yanaendelea karibu na mji ulioko mpakani wa Gamboru Ngala.
Mapigano hayo yanawadia saa chache tu baada ya
wapiganaji hao wa Boko Haram kutoa kanda ya video ambayo walitangaza
kuundwa kwa himaya ya Kiislamu kaskazini Mashariki mwa Nigeria.
Wanajeshi hao walikuwa wakikabiliana na wapiganaji wa Boko Haram
Kiongozi wa Boko Haram Abubakar Shekau
alizungumza kwenye kanda ya video iliyotolewa ili kupongeza wapiganaji
wake kwa kuchukua udhibiti wa mji wa Gwoza mapema mwezi huu.
Haijabainishwa iwapo Bwana Shekau ameahidi kutii
Muungano wa wapiganaji wa kundi la kiislamu la Islamic State
inayotawala sehemu kubwa ya Kaskazini mwa Iraq na Syria.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria Chris Olukolade
alipinga tangazo hilo akisema kuwa ''hakuna hata nchi moja ya taifa hilo
iliyotwaliwa na kuwa Nigeria ni moja. ''
Kiongozi wa Boko Haram Shekao ametangaza himya ya KIislamu Kaskazini mashariki mwa Nigeria
Maelfu ya watu wameuwawa kaskazini mashariki mwa Nigeria tangu 2009, wakati Boko Haram ilipoanza uasi wake.
Gwoza, iliyokuwa na wakazi 265,000 katika sensa iliyopita, ndiyo mji mkubwa zaidi ulio chini ya utawala wa Boko Haram.
Imepeperusha bendera zake juu ya Kasri ya Emir wa Gwoza, kiongozi wa kiasili wa mji huo, wakazi wanasema
No comments:
Post a Comment