Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ akipozi.
Msanii wa filamu, Salma Omary ‘Sabby’ ameamua kufunguka kuwa ameteswa sana na rushwa ya ngono aliyokuwa akikutana nayo pindi alipokuwa akifurukuta kutoka kisanii.Akizungumza na Ijumaa Sabby alisema, tatizo hilo la rushwa anaweza kuwa miongoni
mwa wasanii waliosumbuliwa sana wakati kuna baadhi walipokuwa
wakitolewa nje, walikuwa wanajenga bifu naye na wengine kumtishia
kumharibia.
“Mimi
kitu ambacho kinaniumiza sana mpaka leo ni jinsi wanawake
tunavyodhalilishwa kila siku, naumia mno nimepita katika tabu nyingi
mpaka nafikia hapa leo, ila namshukuru Mungu siku zote,”
alisema Sabby ambaye ameng’ara kwenye filamu kama vile Siri ya Gining, Hard Price, Moto wa Radi, Dr. Ray na nyinginezo.
No comments:
Post a Comment