Kigoma. Polisi mkoani Kigoma, wamewaua watu watano wanaosadikiwa
kuwa majambazi waliokuwa katika harakati za kufanya unyang’anyi wa
kutumia silaha kwa kuteka magari ya abiria mkoani humo.
Taarifa hiyo imetolewa jana na Kamanda wa Polisi
Mkoa wa Kigoma, Jafari Mohamed ilisema tukio hilo lilitokea Septemba 3,
2014 saa 11 alfajiri katika pori la Malagarasi Wilaya ya Kasulu.
Kamanda Mohamed alisema polisi imewaua majambazi
hao baada ya msako mkali uliotokana na tukio la awali la kutekwa na
kulipuliwa kwa bomu basi dogo la abiria aina ya Toyota Hiace lililokuwa
likitokea Kata ya Kilelema.
Alisema Agosti 27, walipata taarifa za kuwapo majambazi kutoka nchi jirani ya Burundi wakijiandaa uhalifu.
“Baada ya kupata taarifa, tuliweka mtego katika
eneo lililokusudiwa kufanyika uhalifu na muda uliokusudiwa majambazi
hao, walifika eneo hilo na walipoona dalili za kukamatwa na askari,
walianza kufyatua risasi ovyo na askari wakiwa katika harakati za
mapambano waliyaua majambazi hayo,” alisema.
Alisema majambazi hao walikutwa na mabomu matatu ya kutupwa kwa mkono.
No comments:
Post a Comment