welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Wednesday, 17 September 2014

Rais Kikwete aenda Marekani

RAISI JAKAYA KIKWETE
Rais Jakaya Kikwete ameondoka Jumatatu usiku kwenda Marekani kuanza ziara ya wiki mbili nchini humo.
Taarifa iliyotolewa jana na Kurugenzi ya Mawasiliano, Ikulu, ilisema Rais atahutubia Mkutano wa 69 wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mjini New York pamoja na kuhudhuria mikutano muhimu Washington, D.C.
Akiwa Mjini New York, Rais Kikwete atashiriki katika mikutano mikubwa zaidi ya 10 iliyopangwa kufanyika Septemba 24 hadi Oktoba Mosi. Rais Kikwete amepangwa kuwa kiongozi wa 12 duniani kuhutubia baraza hilo.
Septemba 25. Pia atakuwa mwenyekiti wa Kamati ya Wakuu wa Nchi Wanachama wa Umoja wa Afrika (AU) kuhusu mazingira (CAHOSC) ulioitishwa na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN), Ban Ki Moon.

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...