![]() |
Yaya Sanogo afunga bao lake la kwanza katika mechi dhidi ya Borussia Dortmund .Arsenal ilishinda kwa mabao 2-0 |
Yaya Sanogo aliifungia Arsenal bao
lake la kwanza walipoizaba kilabu ya Borusia Dortmund na kuhakikisha
wamefuzu katika hatua ya muondoano wa michuano ya kombe la kilabu bingwa
barani Ulaya.
Mshambuliaji huyo wa miaka 21 alifunga bao hilo
baada ya kushiriki katika mechi 19 bila bao lolote alipomaliza pasi kati
yake na Santi carzola mda mchache tu baada ya mechi kuanza.
Alexis Sanchez alifanya mambo kuwa 2-0 baada ya mda wa mapumziko alipopachika bao lililowaacha wengi vinywa wazi.
Vilevile
mlinda Lango wa Dortmung aliokoa shambulizi la Sanchez mda mchache
baadaye, huku shambulizi jengine la kiungo wa kati wa Arsenal Alex
Oxlaide Chamberlain likigonga chuma cha goli.
Arsenal kwa mara ya
kwanza walionyesha mchezo uliokomaa huku mabeki wake waliolaumiwa kwa
msururu wa matokeo mabaya wakijitahidi vilivyo.
Wachezaji hao
waliwazuia washambuliaji wa Dortmund akiwemo Pierre Aubemayang ambaye
alikuwa moto wa kuotoa mbali wakati timu hizo mbili zilipokutana kwa
mechi yao ya kwanza nchini Ujerumani.
Wakati huohuo Mkufunzi wa timu ya Liverpool Brendan Rodgers amesema
kuwa amefurahishwa na hatua ya timu yake kuchukua udhibiti wa hatma yao
hadi mechi ya mwisho katika michuano ya kufuzu kwa raundi za muondoano
wa ligi ya kilabu bingwa Ulaya.
Timu hiyo ilifungwa bao la pili
katika mda wa majeruhi na kilabu ya Bulgaria Ludogorets na kutoka sare
ya 2-2 lakini bado watafuzu katika michuano ya raundi ya maondoano iwapo
wataifunga timu ya Bacel mwezi Ujao.
Katika matokeo mengine:
Atl Madrid 4 - 0 Olympiakos
Malmö FF 0 - 2 Juventus
FC Basel 0 - 1 Real Madrid
Zenit St P 1 - 0 Benfica
Bayer Levkn 0 - 1 Monaco
Anderlecht 2 - 0 Galatasaray
No comments:
Post a Comment