![]() |
Steven Gerrard na kocha Brenda Rodgers. |
Nahodha wa kilabu ya Liverpool
Steven Gerad amepinga kuwepo kwa mzozano wowote kati yake na mkufunzi wa
timu hiyo Brendan Rodgers baada ya kuwachwa nje katika mechi kati ya
Liverpool na Stoke City.
Ilikuwa mara ya kwanza kwa kiungo huyo wa kati kuwachwa nje tangu mwaka mpya wakati alipokuwa na jeraha.
Hatua
hiyo ya Rodgers ya kumwacha nje Gerrad inajiri wakati ambapo nahodha
huyo alikuwa anasherehekea miaka 16 tangu ajiunge na timu hiyo.
lakini alisema katika Instagram kwamba mazungumzo ya vyombo vya habari ni ya upuuzi na kwamba hakuna mgogoro wowote kati yao.
Rodgers
alikiri kwamba hakujuwa iwapo Gerrad alikuwa anasherehekea kujiunga na
kilabu hiyo alipomuwacha nje wakati timu hiyo ilipopata ushindi wa 1-0
katika uwanja wa Anfield.
No comments:
Post a Comment