![]() |
Spika wa bunge la Tanzania Anne Makinda |
Speaker wa Tanzania Anne Makinda ameshtumiwa kwa kujaribu kuwatetea wale wanaodaiwa kuhusika katika kashfa ya ufisadi ya Escrow.
Kulingana
na wachambuzi,wasomi na wataalam wa sheria hatua yake ya kujenga
mazingira ya kuwapendelea washukiwa huenda ikasaidia kuwalinda watu hao.
Wakili
maarufu mjini Daresalaam Sylvanus Sylivand ameliambia gazeti la the
Citizen kwamba spika makinda alitarajiwa kufuata mfano mzuri uliowekwa
na wenzake katika kashfa za awali ambapo bunge lina uwezo wa
kuwashinikiza mawaziri na waziri mkuu kujiuzulu.
Ni wazi kwamba
bunge linaweza kuishauri serikali kuwachukulia hatua viongozi
wanaoshukiwa lakini si lazima kwamba rais afuate agizo hilo.
Kulingana
na Sylivand,ni wazi kwamba kuna kitu kinachofichwa ili kuendesha ajenda
tofauti ambayo itasadia aibu iliopata serikali.
Muhadhiri wa chuo kikuu cha Dodoma Paul Loisulie amesema kuwa bunge sharti lichukue hatua kama taasisi.
''Kile ambacho kimetokea bungeni kuna uwezekano mkubwa kitaligawanya bunge na wananchi.''.
Inaonekana
kwamba baadhi ya wabunge wa CCM wanajaribu wawezalo kuwatetea viongozi
wanaoshukiwa bila kujali maslahi ya raia walio masikini.
Julius
Mtatiro wa Chama cha Civic Front amesema kuwa CCM inataka kuwalinda
viongozi wake wakuu ili raia wasielewe kuhusu kilichotokea baada ya
Spika Makinda kuwataka baadhi ya washukiwa hao kupendekeza hatua ambazo
zingefaa kuchukuliwa dhidi yao.
Kulingana na Profesa Kitila wa
Chuo kikuu cha Dar es Salaam Wabunge wana uwezo wa kuwaweka katika
mizani watu watatu pekee ,rais,waziri mkuu na Spika na kile kilichokuwa
kikendelea bungeni ni fursa ya wananchi kufikiria sana kabla ya
kuipitisha katiba mpya.
No comments:
Post a Comment