![]() |
Mizengo Pinda waziri mkuu wa Tanzania ametajwa kwenye ripoti hiyo iliyowasilishwa bungeni |
Ripoti ya Kamati ya bunge ya Hesabu za Serikali imewataja baadhi ya vigogo wanaohusika na kashfa ya IPTL Nchini Tanzania akiwemo Waziri Mkuu na kuwataka kuwajibika kisiasa na kisheria.
Sakata hiyo ya IPTL inahusihswa na upotevu wa mamilioni
ya fedha na kwa muda mrefu umezusha mjadala mzito katika bunge la
Tanzania.
Katika ripoti hiyo iliyowasilishwa na mwenyekiti wa
kamati hiyo Zitto Kabwe na makamu mwenyekiti Deo Filikunjombe,
imethibitisha kuwepo mazingira ya udanganyifu na ufisadi katika mchakato
wa malipo yaliyofanyika na kueleza kuwa upotevu huo wa fedha ungeweza
kudhibitiwa kama kungekuwa na uwajibikaji wa kutosha kwa baadhi ya
viongozi.
Kamati hiyo imewataja viongozi wengine wanaotakiwa kuwajibika
kutokana na kashfa hiyo kuwa ni mwanasheria,Waziri wa nishati na Madini,
Naibu Waziri wa Nishati pamoja na viongozi wengine wa bodi.
Ripoti
hiyo ilitokana na ukaguzi uliofanywa na Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Hesabu za Serikali (CAG) ambayo ilianika ukiukwaji mkubwa wa taratibu
wakati wa uchotaji wa fedha hizo pia mahojiano na mkurugenzi mkuu wa
Takukuru na Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA).
Waziri Pinda
amelimbikizwa lawama ikidaiwa kuwa alijua kuwapo kwa ufisadi huo na
matamshi yake kuwa fedha hizo hazikuwa mali ya umma, wakati Mwanasheria
Mkuu Jaji Frederick Werema ameonekana kutoishauri vizuri Serikali na pia
kuagiza fedha hizo zitolewe kwenye akaunti hiyo.
Waziri Sospeter
Muhongo amelaumiwa kwa kukosa kuchukua hatua wakati akijua kuwapo kwa
sakata hilo, huku naibu wake, Stephen Masele akitiwa hatiani kwa
kulidanganya Bunge.
Kashfa nyingine zilizowahi chukua uzito mkubwa
katika bunge la Tanzania na kusababisha viongozi kuwajibika wakiwemo
Waziri Mkuu ni pamoja na kashafa ya Richmond,EPA na sasa hii ya ESCROW
ambayo kwa mara nyingine kamati hiyo imeonyesha wazi mapendekezo yake ya
kutaka kuwajibika kwa waziri mkuu, Mawaziri na viongozi wengine.
No comments:
Post a Comment