![]() |
Berry na aliyekuwa mumewe Gabriel Aubry |
Muigizaji maarufu wa Marekani Halle
Berry, ameghadhabishwa mno na hatua ya aliyekuwa mumewe juu ya
kumbadilisha mwanawe rangi ya ngozi pamoja na kuweka kemikali kwenye
nywele zake ili ziwe singa.
Muigizaji huyo alikasirishwa na jambo
hilo kwani mwanawe mwenye umri wa miaka sita Nahla Berry ambaye kawaida
anakuwa na nywele koto ameanza kubadilika.
Hapo ndipo hasira
zilimpanda Halle Beryy kiasi cha kumpeleka mahakamani babake mtoto huyo
Gabriel Aubry waliyeachana naye mwaka 2010.
Berry alinukuliwa
akisema,'' kila siku wasiwasi unanizidi kuhusu athari atakazopata
mwanangu Nahla kisaikolojia na kimwili kwa kuwekewa kemikali kwa nywele.
Pia ataathirika kimawazo kutokana na mwili wake kuanza kubadilishwa.''
Pamoja
na taarifa yake Berry aliweka picha za mwanawe za kabla na sasa ili
kuonyesha jinsi mwanawe alivyobadilishwa rangi yake ya mwili huku nywele
zake zikiwekwa kemikali ili kuwa singa.
''Nataka mahakama kumuamuri babake mtoto huyu Gabriel kukoma juhudi
zake za kubadilisha mwonekano wa mtoto wetu na labda kumsababisha mtoto
kuanza kujiuliza kwa nini rangi nyeusi ya ngozi yake sio nzuri au
haifai.
Kesi hiyo iliwasilishwa mahakamani Jumatatu na wakili wa
Berry ambaye hakufika mahakamani. Inaarifiwa jaji jaji aliamuru kwamba
kuanzia sasa, babake Nahla lazima akome kumbadilisha mwonekeno wa mtoto.
Halle
Berry na Aubry waliachana mwaka 2010 na jaji aliamua kuwa wote wawili
hawana ruhusa ya kubadilisha sura na mwonekano wa mtoto wao kivyovyote.
Kwa
mujibu wa jarida la TMZ, Halle Berry anahofia kuwa Aubry anajaribu
kumfanya mwanawe kuwa mweupe na kwamba hataki afanane kama Mmarekani
mweusi.
Hapo awali, Berry mwenyewe alisema kuwa mwanawe ni
marekani mweusi kama yeye mwenyewe. Babake mtoto buyo ana asili
mchanganyiko ya Canada na Ufaransa
No comments:
Post a Comment