![]() |
Afisa wa polisi akishikilia bendera inayodaiwa kuwa ya makundi mashirika ya kigaidi iliopatikana ndani ya msikiti mmoja |
Misikiti minne iliofungwa na maafisa
wa polisi wiki iliopita baada ya kuchukuliwa na vijana wenye itikadi
kali za kiislamu hatimaye imefunguliwa.
Hatua ya kuifungua
misikiti hiyo ya Minaa,Sakina,Musa na Swafaa inajiri baada ya siku mbili
za mazungumzo kati ya viongozi wakuu wa kiislamu,wataalam na uongozi wa
kaunti ya Mombasa.
Maelezo ya mazungumzo hayo yalioandaliwa na Gavana wa Mombasa Hassan Joho na kaunti kamishna Nelson Marwa yamefanywa kuwa siri.
Kabla
ya misikiti hiyo kufunguliwa ,viongozi wa kiislamu pamoja na wataalam
walilazimika kuajiri kiongozi wa dini wa kila msikiti na kubuni kamati
maalum ya kusimamia misikiti hiyo ya kisauni na majengo mjini Mombasa.
''Hatutaki wajisikie kana kwamba serikali ina wakandamiza.Tumewapa
mda wa kuzungumza na kuamua kuhusu kamati za misikii hiyo na viongozi w
dini ambao watakuwa wakisimamia ibada.Watatupatia majina na kufikia
kesho{leo} misikiti hiyo itafunguliwa'',alisema bwana Marwa ambaye ndio
mwenyekiti wa kamati ya usalama kaunti ya Mombasa.
Duru zinaarifu
kuwa miongoni mwa wale walioalikwa katika mazungumzo hayo ni viongozi
wakuu wa kiislamu wakiwemo wawakilishi kutoka baraza kuu la waislamu
nchini Kenya SUPKEM,barasa kuu la ushauri wa maswala ya kiislamu na
baraza la maimamu na wahubiri nchini Kenya CIPK.
Misikiti hiyo
ilifungwa wiki iliopita na maafisa wa usalama baada ya uvamizi katika
Msikiti wa Musa pamoja na msako wa kuwanasa zaidi ya watu 250 ambao
baadaye walishtakiwa kwa kuwa wanachama wa makundi ya kigaidi.
Maafisa wa polisi pia walionyesha baadhi ya silaha na nakala ambazo wanasema zilipatikana katika msikiti huo.
Muda
mchache baada ya kukamatwa kwao,magenge ya vijana walizua ghasia na
kuanza kuwashambulia raia wasio kuwa na hatia katika vituo vitatu vya
mabasi pamoja na makaazi katika eneo la kisauni.
Wakati wa ghasia hizo watu watatu walidungwa visu na kufariki huku wengine saba wakijeruhiwa vibaya.
Viongozi
wa kiislamu mjini Mombasa na maeneo mengine ya nchi wamekuwa wakitaka
kufunguliwa kwa misikiti hiyo ambayo imekuwa katikati ya utata kuhusu
madai kwamba ilikuwa inatumiwa kuwafunza vijana itikadi kali mbali na
kuhifadhi silaha kinyume na sheria.
No comments:
Post a Comment