![]() |
Wayne Rooney afurahia baada ya kufunga bao la pili dhidi ya timu ya Hull City |
Mkufunzi Gus Poyet aliihangaisha
timu ya Chelsea na kuwajaribu viongozi hao wa Ligi kupitia mchezo mzuru
wa timu yake Sunderland.
Chelsea ilishindwa kuliona lango la Sunderland kupitia ngome mahsusi ya Sunderland iliowazuia washambuliaji wake.
Shambulizi
kali ambalo nusra liiweke Chelsea kifua Mbele ni lile lakKiungo wa kati
Willian ambalo liligonga chuma cha goli na kutoka nje.
Hatahivyo
Mshambuliaji wa Sunderland pia naye alipiga mkwaju mkali uliogonga chuma
cha goli la Chelsea huku Sunderland ikidhibiti safu ya kati na
kuimarisha mashambulizi yake katika ngome ya Chelsea.
Mchezo huo ulikamilika na sare ya bila kwa bila na kuifanya
Sunderland kuwa timu ya kwanza kuwazuia viongozi hao wa Ligi kufunga
tangu msimu huu uanze.
Katika matokeo mengine Arsenal ilizuia kupoteza kwa mara ya tatu mafululizo pale walipoishinda West Brom ugenini.
The
Gunners kama wanavyojulikana walianza mechi hiyo wakiwa na alama za
chini zaidi baada ya kucheza mechi 12 katika kipindi cha miaka 32,lakini
cichwa kizito cha mshambuliaji Danny Welbeck, kilihakikisha vijana wa
Arsene Wenger wanatia kibindoni alama tatu.
Katika uwanja wa Old Trafford,bao la Robbin Van Persie Robin
liliimarisha ushindi wa Manchester United dhidi ya Hull City na kuzima
midomo ya wale waliokuwa wakijiuliza maswali mengi kuhusu hali ya
mchezaji huyo msimu huu.
Miongoni mwa wakaosoaji wake ni kocha
Louis Van Gaal ambaye aliyemuorodhesha mshambuliaji huyo katika mechi
hiyo licha ya kudai kwamba alikuwa na mchezo m'baya wakati wa mechi kati
ya Arsenal na Manchester wikendi iliopita.
Manchester United ilipata ushindi wa mabao 3-0 kupitia wachezaji wake Chris Smalling na nahodha Wayne Rooney.
katika matokeo mengine
Burnley 1 - 1 Aston Villa
Liverpool 1 - 0 Stoke
QPR 3 - 2 Leicester
Swansea 1 - 1 Crystal Palace
West Ham 1 - 0 Newcastle
No comments:
Post a Comment