welcome

Your welcome to Leyla Nyenzi Blog, Dodoma-Tanzania, for the only latest Audio's,Video's,Photo's, Events and Advertisement.

Sunday, 30 November 2014

Raia wa Misri waandamana kufuatia kuondolewa mashtaka kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Hosni Mubarak

Raia wa Misri waandamana kufuatia kuondolewa mashtaka kwa aliyekuwa rais wa taifa hilo Hosni Mubarak
Vikosi vya usalama nchini Misri vimepambana na karibu waandamanaji 2000 karibu na eneo la Tahrir Square mjini Cairo ambapo mtu mmoja aliuawa.
Maandamano hayo yanafanyika kufuatia uamuzi wa mahakama wa kumuondolea mashtaka aliyekuwa rais wa Misri Honi Mubarak kuhusiana na mauaji ya zaidi ya waandamanaji 200 wakati wa maandamano ya mwaka 2011.
Kweye mahojiano na kituo kimoja cha runinga baada ya hukumu hiyo bwana Mubarak alisema kuwa hajafanya lolote baya.
Awali alihukumiwa kifungo cha maisha gerezani lakini hukumu hyo ikabatilishwa .
Hata hivyo bado yuko kuzuizini baada ya kupatikana na makosa ya ufujaji wa pesa za umma

No comments:

Post a Comment

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia mkito.com!

Kuwa wa kwanza kupata ladha kutoka kwa wakali wa huu muziki Afrika Kusini kupitia  mkito.com !  Bila shaka utakuwa umeusikia huu wimbo kw...