![]() |
BALOTELLI |
Shirikisho la soka FA linachunguza
ujumbe wa Instagram wa mshambuliaji wa Liverpool Mario Balotelli
unaodaiwa kuwa ni wa kibaguzi.
Ballotel mwenye umri wa miaka 24
akijibu shutma dhidi yake kutokana na ujumbe wake mtandaoni aliandika
tena ujumbe usemao “mama yangu ni Myahudi wote nyamazeni kimya”.
Hata hivyo Balotelli anadaiwa kuufuta haraka haraka ujumbe wa awali aliouandika ambao unadaiwa kuwa ni wakibaguzi.
Msemaji
wa Liverpool anayochezea Balotell amesema kuwa wanataarifa kuhusiana na
ujumbe huo na kwamba watafanya mazungumzo na Balotell.
Shirikisho
la soka FA limesema kuwa linataarifa kuhusiana na mchezaji huyo kuiweka
taarifa hiyo katika Instagram na kisha kuifuta baadae.
Mkurugwenzi wa zamani wa shirikisho la soka Simon Johnson anasema Balotell anastahili kuchukuliwa adhabu kwa kitendo hicho. SOURCE: BBC SWAHILI
No comments:
Post a Comment