![]() |
DIAMOND PLATNUMZ |
Mwanamuziki mwenye sifa kedekede
nchini Tanzania, Naseeb Abdul, kwa jina lengine, 'Diamond Platnumz',
anaendelea kujizolea sifa kimataifa baada ya kushinda tuzo tatu za
Channel O African Music Awards.
Tamasha lilifanyika nchini Afrika Kusini mwishoni mwa wiki.
Diamond
alijizolea tuzo tatu, ikiwemo ya mwanamuziki mgeni mwenye kipawa
kikubwa, mwanamuziki bora zaidi kwenye mtindo wa Afro-Pop na tuzo ya
mwanamziki bora zaidi katika kanda ya Afrika Mashariki.
Diamond anajulikana kama
mwanamuziki anaeenziwa zaidi nchini Tanzania na alishinda tuzo hizo kwa
wimbo wake 'Number One', na kuwabwaga wanamuziki wengine wanaosifika
kikanda na kimataifa.
Hii ni mara ya pili mwaka huu kwa Diamond
ambaye mwezi Mei alishinda tuzo saba katika mashindano mangine ya
wanamuziki ikiwemo mwanamuziki bora zaidi wa kiume , mwandishi na mtunzi
bora zaidi wa nyimbo pamoja na mtumbuizaji bora zaidi Tanzania.
Mwanamuziki
Tiwatope Savaga wa Nigeria naye alijinyakulia tuzo ya mwanamuziki bora
zaidi wa kike hasa kwa vile alivyoimba kibao chake 'Eminado'.
Tuzo hizo huandaliwa na kituo cha televisheni ambacho hucheza tu muziki cha Channel O.
No comments:
Post a Comment