Polisi nchini Misri wamelazimika
kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya waandamanaji wanaopinga hatua ya
mahakama nchini humo kutupilia mbali kesi ya mauaji dhidi ya Rais
aliyeondolewa madarakani Hosni Mubarak.
Zaidi ya watu 2000
walikusanyika katika viunga vya Tahrir mahala ambapo ndipo zilipozaliwa
harakati za mapinduzi ya nchi hiyo mwaka 2011.
Awali Mubarak
alihukumiwa kifungo cha maisha jela ambapo kwa sasa anatumikia pia
kifungo cha miaka mitatu kwa makosa ya matumizi mabaya ya fedha za umma.
Kwa sasa Hosni Mubarack anashikiliwa katika hospitali ya jeshi ambako pia anapatiwa matibabu.
Waziri
wake wa zamani wa mamabo ya ndani Habib al-Adly na wenzake sita
walihukumiwa kifungo cha maisha 2012, inakadiriwa takriban watu 800
waliuawa wakati wa harakati za kumuondoa kiongozi huyo Februari 11.2011.
No comments:
Post a Comment