![]() |
waziri wa Ulinzi Edgar Lungu |
Mahakama kuu nchini Zambia
imetangaza kuwa waziri wa Ulinzi Edgar Lungu ndio atakeyewania wadhfa wa
Urais kupitia tiketi ya chama cha Patriotic Front katika uchaguzi wa
mwezi Ujao.
Chama cha Patritic Front kimegawanyika kuhusu ni nani atakayekrithi rais sata kufuatia kifo chake.
Mgawanyiko huo utafungua njia kwa upinzani kuchukua mamlaka katika uchaguzi huo kulingana na wachambuzi.
Makundi
pinzani ya chama cha PF yalifanya mikutano tofauti katika kipindi cha
juma moja ili kumchagua mgombea wa urais katika uchaguzi huo wa january
20.
Upande wa bwana Lungu ulipinga uteuzi wa Bwana Sampa mahakamani.
''Mkutano
wa chama unaodaiwa kufanyika Disemba mosi ambapo mheshimiwa Miles sampa
anadaiwa kuchaguliwa kama mgombea wa chama cha Patritic Front nataka
kutangaza kwamba ni haramu na uamuzi wote ulioafikiwa si wa
halkali'',Jaji aliamuru.
Bwana sampa amesema kuwa atakataa rufaa dhidi ya uamuzi huo.
Kiongozi
huyo ni mshirika wa karibu wa kaimu rais Guy Scott ambaye alichungua
mamlka baada ya kifo cha Sata katika hospitali ya Uingereza mnamo mwezi
Octoba akiwa na umri wa miaka 77.
Bwana Scott alichukua jukumu
muhimu katika mgogoro wa kuwania mamlaka alipomuondoa kwa mda bwana
Lungu kama katibu mkuu wa chama hicho mda mchache baada ya kifo cha
Sata.
Hatahivyo alilazimika kurudisha bwana Lungu siku moja baadaye kufuatia lalama katika chama.
Bwana Scott ambaye hawezi kupigania urais anajaribu kuwa mtu muhimu katika siasa za taifa hilo kulingana na wachambuzi..
No comments:
Post a Comment