![]() |
Putin akitoa hotuba yake kwa taifa kupitia televishen |
Rais Vladmir Putni wa Urusi ametumia
hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa kushambulia mataifa ya Magharibi
ambayo amesema yamekuwa na unafiki mkubwa juu ya hali ilivyo nchini
Ukraine.
Bwana Putin alisema kuwa kama pasingekuwa na matatizo
Ukraine wakati huu mataifa ya Magharibi bado yangalikuja na swala
lingine la kujaribu kudhibiti Urusi.
Alisema pia kuwa Urusi haitakubali kusambaratika jinsi ilivyofanyika katika taifa la Yugoslavia.
Bwana
Putni alisema kuwa Uchurmi wa Urusi unakabiliwa na changamoto nyingi
siku za mbeleni, lakini akasisitiza kuwa vikwazo hivyo vitasaidia Urusi
kuunda mbinu mwafaka za kujitegemea.
Rais aliwahimiza waekezaji
kurudi tena Urusi kwa kutangaza kuwa hakutakuwepo na upekuzi juu ya
uhalifu wa fedha au kama kulikuwepo na wizi wa kodi juu ya rasilmali
itakayoingizwa nchini.
Alisema Urusi ni mahali salama zaidi kwa Warusi kuhifadhi pesa zao.
No comments:
Post a Comment