![]() |
Mwigizaji Gauhar Khan |
Mwigizaji maarufu wa Bollywood
ambaye pia ni mwanamitindo, Gauhar Khan, alizabwa kofi wakati wa
shughuli ya kurekodi makala ya kipindi kuhusu maisha yake.
Mwigizaji huyo alizabwa kofi na mmoja wa waliokuwa wanatazama kipindi hicho eti kwa kuwa alikuwa amevalia nguo fupi sana.
Polisi
walimkamata mwanamume mwenye umri a miaka 24 kwa kumshambulia mwigizaji
huyo wakati wa kurekodi kipindi kijulikanacho kama , ''India's Raw
Star'' mjini Mumbai.
Mwanamume aliyemshambua muigizaji huyo
alinukuliwa akimkaripia na kumwambia, kwamba kwa kuwa yeye ni mwanamke
wa kiisilamu hapaswi kuvalia nguo fupi kama ile.
Mwanamume huyo alitarajiwa kufikishwa mahakamani Jumatatu.
Tukio hilo lilitokea Jumapili, wakati wa kurekodiwa kwa makala ya mwisho ya kipindi hicho.
Uchunguzi
umeonyesha kuwa mtu mmoja kutoka kwa mashabiki, alianza kumkejeli Khan
ambaye naye hakumsaza kwani alianza kujibizana naye. Katika majibizano
yao, mwanamume huyo alimzaba kofi Khan.
Duru zinasema kuwa walinzi waliokuwa katika eneo hiloi walimshinda nguvu mwanamume huyo ambayo walimkabidhi kwa polisi.
Polisi
walimshitaki mwanamume huyo kwa kitendo cha kumzaba kofi Khan ambaye
ameigiza katika filamu nyingi tu ikiwemo, 'Rocket Singh: Salesman of the
Year.'
chanzo: bbc swahili
No comments:
Post a Comment